Ugonjwa wa Corona waibuka Mashariki ya kati

18 Oktoba 2013

Shirika la afya ulimwenguni WHO limefahamishwa kuhusiana kuzuka kwa ugonjwa wa matatizo ya kupumua unaosababishwa na virusi vya Corona ambao umeikumba nchi ya Qatar.

Tayari mtu mmoja mwenye umri wa miaka 61 ambaye amekubwa na tatizo hilo amelazwa katika hospitali moja tangu Oktoba 11 akipatiwa matibabu ya karibu.

Vipimo vilivyochukuliwa na baadaye kujaribiwa katika maabara huko nchini Uingereza vimethibitisha juu ya tatizo hilo.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mtu huyo hajawahi kutoka nje ya Qatar katika kipindi cha wiki mbili zilizopita kabla hajaanza kuugua.

Mgonjwa huyo anamiliki shamba kwamba na kutokana na mazingira ya kazi yake atasadikika atakuwa amekutana na mifugo ikiwemo ngamia, kondoo na kuku.