Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lapata wanachama 5 wapya wasio wa kudumu

Baraza la Usalama lapata wanachama 5 wapya wasio wa kudumu

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, leo limepiga kura kuwachagua wanachama watano wapya wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama. Joshua Mmali ana habari zaidi kuwahusu wanachama hao.

(TAARIFA YA JOSHUA)

Nigeria, Chad, Saudi Arabia, Lithuania na Chile ndio wanachama wapya wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama. Rais wa Baraza Kuu, John William Ashe, ametangaza matokeo hayo:

 (SAUTI YA ASHE)

 Nigeria, Chad na Saudi Arabia zitawakilisha bara Afrika na Asia-Pasifiki,Lithuania itawakilisha Mashariki mwa Ulaya, na Chile, ikiwakilisha Amerika ya Kusini.

Nchi nyingine zilizoshiriki kura hiyo ni Senegal, Gambia na Croatia ambazo hazikupata kura za kutosha.

Wanachama wasio wa kudumu kwenye Baraza la Usalama hawana mamlaka ya kura ya veto, au kupinga maamuzi. Wanachama wengine wasio wa kudumu ambao watasalia kwenye Baraza la Usalama kwa mwaka huu ni Argentina, Australia, Luxembourg,  Jamhuri ya Korea na Rwanda. Wanachama wa Kudumu kwenye Baraza la Usalama ni Marekani, Uchina, Ufaransa, Uingereza na Urusi.