Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa kufanyika Addis Ababa wiki ijayo

Mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa kufanyika Addis Ababa wiki ijayo

Suala la kuwepo kwa hali bora ya hewa na huduma za hali ya hewa ili kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa na maendeleo endelevu ni kati ya masuala ambayo yatajadiliwa kwenye mkutano wa tatu kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na maendeleo barani Afrika ambao utaandaliwa mjiji Addis Ababa nchini Ethiopia kuanza tarehe 21 hadi 23 mwezi huu . Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Ukiwa umeandaliwa na kituoa kinachohusika na sera kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa chini ya mpango wa hali ya hewa kwa mandeleo kauli mbiu ya mkutano huo ikiwa ni kusimama: fursa zitokazo na mabadilko ya hali ya hewa zinaweza kuchangia maendelo barani? Muungano wa Afrika AU na Shirika la utabiri wa hewa duniani WMO watafanya mkutano wa pembeni ambao utazungumzia mianya iliyopo na mahitaji ya siku za baadaye katika utoaji wa huduma zinazohusiana na hali ya hewa. Mkutano huo pia utajadili mahitaji ya uongozi wa kisiasa na ushirikiono ili koboresha huduma za mazingira na hali ya hewa katika utoaji uamuzi kwenye sekta muhimu kama sekta ya kilimo, maji na usafiri