Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katika siku ya kupunguza majanga dunia, UM wawaangazia watu wenye ulemavu

Katika siku ya kupunguza majanga dunia, UM wawaangazia watu wenye ulemavu

Katika kilele cha kuadhimisha siku za kupunguza majanga duniani, inayoadhimishwa kila Oktoba 13,Umoja wa Mataifa umezitolea wito nchi wanachama kuhakikisha zinatoa usalama kwa watu wenye ulemavu ikiwemo kuwashirikisha katika mipango pamoja na dhana za uokoji.

Katika ujumbe wake siku hiyo, Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema kuwa jambo linalopaswa kuzingatiwa ni kuhakikisha kwamba mifumo yote ya uokoaji ,kampeni ya uletaji uelewa juu ya maonyo ya mapema inapaswa kuzingatia makundi ya watu wasiojiweza.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha kwa kauli moja hapo mwaka 2009 kuwa Oktoba 13 ni siku ya kimataifa ya kupunguza majanga, na kuiondosha siku iliyokuwa aikidhimishwa hapo awali.

Miongoni mwa mambo yanayozingatiwa wakati wa siku hiyo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana namna wanavyoweza kuwajibika kupunguza majanga.

Inakadiriwa kwamba zaidi ya watu bilioni moja wanaishi katika hali ya ulemavu na ujumbe wa mwaka huu ulilenga kuwamulika watu hao .