Kitendo cha Guatemala kudai sehemu ya Belize ni tishio:

30 Septemba 2013

Moja ya masuala yanayopewa kipaumbele katika ajenda za nyumbani na serikali ya Belize ni kupatia ufumbuzi dai la Guatemala la kudai sehemu ya mamlaka ya Belize amesema waziri wa mambo ya nje wa Belize Wilfered Elringtoold .

Akizungumza kwenye mjadala wa baraza kuu Jumatatu bwana Elrington amesema madai hayo ynaweka tishio kwa taifa na yanahitaji kupatiwa suluhu mara moja endapo watu wa nchi zote mbili na ukanda mzima wanataka kuendelea kufurahia kukaa kwa amani hali ambayo imekuwa ikitanabaisha uhusiano wao hadi sasa.

Ameongeza kuwa dai hilo la Guatemala ni chanzo cha hofu kwa raia wa Belize pamoja na wawekezaji nchini humo.

(SAUTI YA ELRINGTON)

“ Zaidi ya hayo maeneo yetu wote ya mipakani yamekuwa yakiathirika na kutokana na shughuli haramu zinazofanywa na Waguatemala wavuvi na wahalifu wengine wnaojihusisha na usafirishaji wa narco, usafirishaji haramu wa watu,ukataji haramu wa mbao, utafutaji haramu wa dhahabu, uchimbaji wamimea ya xate na mingine ya kigeniuporaji wa magofu ya kale ya Mayan. Ukataji haramu wa mbao katika misitu yetu unachangia kuathiri milima yetu na matokeo yake husababisha mafuriko makubwa wakati wa msimu wa mvua na hivyo kupeleka udongo wenye rutuba baharini.”

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter