Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya Haki za binadamu yakaribisha sheria mpya ya haki nchini Libya

Ofisi ya Haki za binadamu yakaribisha sheria mpya ya haki nchini Libya

Ofisi ya haki za binadamu imekaribisha sheria mpya iliyopitishwa nchini Libya ambayo ambayo inakarinisha kipindi cha mpito kwa taifa hilo.

Sheria hiyo inatoa nafasi kuanzishwa tume ya maridhiano itayokuwa na kazi ya kukusanya taarifa zitazisaidia kulivusha taifa hilo linaloandamwa na hali ya mkwamo.

Kupitishwa kwa sheria hiyo sasa kunafungua njia ya kuwepo uwanja wa kuheshimiwa kwa haki za binadamu ambazo kwa kiwango kikubwa zilikiukwa wakati wa utawala wa Muamar Gaddafi

Ofisi hiyo ya haki za binadmu imesema kuwa imepokea kwa furaha kubwa marekebisho hayo kwa vile pamoja na mambo mengine pia imeondoa kipengele kilichokuwa kikitoa kinga kwa wavunjifu wa haki za binadamu wakati wa utawala uliopita.