Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubakaji na mauwaji ni matukio yanayokithiri Syria: Tume ya UM

Ubakaji na mauwaji ni matukio yanayokithiri Syria: Tume ya UM

Tume huru ya kimataifa ya kuchunguza Syriaimesema kuwa mzozo unaoendelea nchini humo umechukua sura tofauti ukihusisha vitendo hatarishi vya uvunjifu wa haki za binadamu, ambavyo vimetekelezwa  na pande zote, serikali na kundi la waasi. George Njogopa na taarifa kamili

(Taarifa ya George)

 

Katika ripoti yake tume hiyo imesema kuwa pande zote mbili zimehusika na matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu ikiwemo, mauwaji ya halaiki, ongezeko la mashambulizi dhidi ya raia.  Ripoti hiyo pia imebainisha kuwepo kwa ongezeko la matukio ya ubakaji, mauwaji, utesaji na uandikiswaji watoto kwenye vikundi vya kijeshi.

Ripoti imefahamisha kuwa watendaji wote wa matukio hayo hawakuwa na hofu yoyote juu ya kuvunja kwa sheria za kimataifa na wakati mwingine walifanya kwa kiburi.

Tume hiyo imesema kuwa kutokana na ukubwa wa madhira hayo, kuna haja kwa pande zote kuzitisha mapigano na kusala suluhu kwa njia ya majadiliano. Paulo Pinheiro, ni Mwenyekiti wa tume hiyo.

(SAUTI YA PINHEIRO)