Mkataba wa kimataifa kuhusu wafanyakazi wa ndani waanza kutumika leo

5 Septemba 2013

Hatimaye mkataba wa kimataifa wa kutetea haki za wafanyakazi wa ndani uliopigiwa chepuo na shirika la kazi duniani, ILO, umeanza kutumika rasmi hii leo na hivyo kupanua wigo wa haki za msingi za wafanyakazi hao. ILO kupitia Mkurugenzi wake wa mazingira ya kazi na usawa, Manuela Tomei inasema hatua ya leo inatuma ujumbe thabiti kwa zaidi ya wafanyakazi wa ndani Milioni 50 duniani kote ambao maisha na mazingira yao ya kazi ni dhalili. George Njogopa na maelezo zaidi.

(Ripoti ya George)

Takwimu za ILO zinaonyesha kuwa hadi sasa kuna jumla ya wafanyakazi za majumbani wanaofikia milioni 53, idadi ambayo haijajumuisha wafanyakazi ambao ni watoto.

Kulingana na hali ya mambo ilivyo idadi hiyo ya wafanyakazi za ndani inasadikika kuongezeka kwa kasi katika nchi zinazoendelea. Inakadiriwa kwamba idadi jumla inaweza kufikia milioni 10.5 iwapo itajumulishwa na watoto ambao wengi wao wanafanya kazi ngumu huku wakiwa na umri usioruhusiwa kufanya kazi. Wanawake ndiyo wanaongoza kwa kuwa watumishi wa ndani.

Wakati mkataba huo wa kimataifa ukianza kufanya kazi rasmi kuanzia leo,habari njema ni kwamba tayari nchi nane zimeridhia kuanza kuutumia. Nchi hizo ni pamoja na Bolivia, Italia,Mauritius, Nicaragua, Paraguay, Philippines, Afrika Kusin na Uruguay.

Tanzaniani mojawapo ya nchia mbazo bado kuridhia mkataba huo na baadhi ya wananchi wake wametoa maoni kuhusu mazingira ya kazi ya wafanyakazi wa ndani.

(VOX POPS)