Mabomu mtawanyiko yatumika nchini Syria

4 Septemba 2013

Wakati madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria yakiwa yanachunguzwa, hii leo kundi la kimataifa linalofanya kampeni ya kupiga vita mabomu ya kutegwa ardhini limechapisha ripoti inayodai kuwa jeshi la Syria linatumia kwa kiasi kikubwa mabomu mtawanyiko kwenye maeneo ya raia. Ripoti ya George Njogopa inafafanua zaidi.

(PKG YA GEORGE NJOGOPA)

Ripoti hiyo iliyochapishwa imefichua ukweli wa mambo ikisema kuwa, katika kipindi cha mwezi Juni mwaka uliopita kulifanyika matukio yaliyoambatana na matumizi ya silaha zilizopigwa marafuku na hivyo kusababisha maafa makubwa kwa wananchi.

Silaha hizo zilizomiminwa kwa wakati mmoja, inasemekana zilitawanywa katika maeneo yanayokadiriwa kufikia 152.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watu walioathirika na matukio hayo walifikia 165

Syria ambayo haijaridhia mkataba wa kimataifa wa upigaji marafuku matumizi ya vishada vya mabomu inakana kutumia silaha hizo zilizopigwa marafuku.

Mary Wareham kutoka shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch ndiye aliyehariri ripoti hiyo.

(SAUTI YA MARY WAREHAM)

Pia tumetegemea taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo mikanda ya video na taarifa nyingine ambazo wananchi wametuma kwenye mitandao ya intaneti.Tunaamini kuwa matumizi hayo huenda yakawa yamepungua lakini hatuna uhakika kuhusiana na hilo. Lakini tunachojua ni kwamba kumekuwa na utumiaji mkubwa wa silaha hizo ambazo zimesababisha maafa.Silaha hizo zimetumika mijini, zimetumika kwenye mashule, zimeuwa watu waliokuwa wakitembea mitaani, vijijini na kadhalika.

Ripoti hiyo pia imetilia shaka uwezekano wa kutumika silaha hizo katika nyingine ikiwemo Myanmar Sudan, Libya na Thailand