Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

AU yakamilisha warsha ya sheria za haki za binadamu kwa jeshi la Somalia:

AU yakamilisha warsha ya sheria za haki za binadamu kwa jeshi la Somalia:

Muungano wa Afrika AU leo umehitimisha mafunzo na warsha yenye lengo la kuboresha uelewa na utekelezaji wa sheria za kimataifa za haki za binadamu kwa maafisa wa jeshi la Somalia.

Warsha na mafunzo hayo yamefadhiliwa na kitengo cha haki za binadamu cha mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM, ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu ICRC.

Warsha na mafunzo hayo yaliyoanza Agost 20 yamefantyika katika awamu mbili yakiwafaidisha maafisa 59. Wakati wa mafunzo maafisa wamefahamishwa kuhusu vipengee muhimu vya sheria za kimataifa za haki za binadamuhususani vile vinavyohusiana na hali ya Somalia, kama kuwalinda raia na waathirika kwenye vita, sheria za mapigano, kuwalinda wafungwa, kuwalinda wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu na vifaa na vitendo vya uhalifu wa vita kwa vita visivyo vya kimataifa na wajibu wa amri zao.

Mwakilishi maalumu wa Muungano wa Afrika na mkuu wa AMISOM balozi Mahamat Saleh Annadif  amekishukuru kitengo cha masuala ya kisiasa cha muungano wa Afrika kwa kufadhili mafunzo hayo na serikali ya Uganda kwa kuwa mwenyeji wa warsha na mafunzo hayo.