Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaendelea na operesheni CAR licha ya usalama kuzorota

WFP yaendelea na operesheni CAR licha ya usalama kuzorota

Huko Jamhuri ya Afrika ya Kati hali ya usalama inaendelea kuzorota kila uchwao lakini hilo halijakatisha tamaa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP katika kusambaza huduma za misaada. WFP inasema kwa wiki kadhaa sasa kumekuwepo na matukio ya uvunjifu wa amani kwenye mji mkuu Bangui na maeneo mengine nchini humo, likitolea mfano tukio la tarehe 21 mwezi huu ambapo waasi wa Seleka walishambulia mji wa mpakani wa Tokyoto na kusababisha mpaka huo kufungwa.

Shirika hilo limesema hivi sasa uhalifu ni tishio kubwa huku watoa misaada wakiwa ni walengwa. Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

 (Sauti ya Byrs)