Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada kwa wakimbizi kutoka Syria walio nchini Iraq yawasili Erbil

Misaada kwa wakimbizi kutoka Syria walio nchini Iraq yawasili Erbil

Ndege ya kukodi ikiwa na vifaa vya misaada kutoka shirika la mpango wa chakula duniani, WFP na lile la wakimbizi, UNHCR imewasili hukoErbil,Iraq. Vifaa hivyo ni pamoja na mahema na biskuti zenye virutubisho na ni kwa ajili ya wakimbizi wa Syria waliokimbilia kaskazini mwa Iraq. Taarifa ya Grace Kaneiya inafafanua zaidi.

(Ripoti ya Grace)

 Zaidi ya wakimbizi 44,000 raia wa Syria wameingia eneo la kikurdi kaskazini mwa Iraq tangu tarehe 15 mwezi Agosti wengi wakiwa ni akina mama na watoto walio kambini huku wengine sasa wakiwa wanaishi na marafiki. Mjumbe wa shirikla la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR nchini Iraq Claire Bourgeois anasema ndege hiyo ilibeba mahema ya kuhudumia familia 340, tani 42 za biskuti na tani 15 za vykaula vingine wakati ambapo idadi ya watu wanaoihama Syria na kuingia Iraq ikizidi kuongezeka. Ndege ya pili inatarajiwa kuwasili Erbil hii leo kutoka Adana nchini Uturuki. Wengi wa wakimbizi waliowasili hivi majuzi wamehamishiwa kambi ya Kawergosk karibu na Erbil ambayo sasa ni makao kwa takriban wakimbizi 15,000.