Bado kuna matumaini kufanyika mkutano wa pili kuhusu Syria: Brahimi
Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu nchiin Syria, Lakhdar Brahimi amesema hali nchini humo inazidi kuzorota kila uchwao na ni vyema pande zote zinazokinzana kufanya mazungumzo na kumaliza mgogoro huo kwa njia ya amani. Bwana Brahimi amesema hakuna upande wowote utakaoibuka na ushindi akiongeza kwamba kadri mzozo huo unavyoendelea,, ndivyo unavyozidi kuwa mgumu na kuongeza machungu kwa wananchi wa Syria. Ameonyesha matumaini yake kuwa Umoja wa Mataifa, MArekani na Urusi zinaweza kukaa pamoja na kukubaliana juu ya mkutano wa pili wa amani waSyria. Khawla Mattar ni msemaji wa Bwana Brahimi.
(Sauti ya Khawla Mattar)
“Bado tuna matumaini ya kuwa na mkutano wa pili wa Geneva, kuhusu Syria. Wawakilishi wake hapa, Damascus na New York, wanafanya kazi kuleta pande zote pamoja kwenye meza ya mazungumzo na kusuluhisha mgogoro kwa njia ya amani kwani hakuna suluhisho kupitia nguvu za kijeshi. Tulichoelezwa na wawakilishi wetu Damascus na wataalamu wengine ni kwamba hakuna upande wowote unaoshinda kwenye vita hivi. Serikali kuna wakati ilisema inashinda, halikadhalika upinzani nao walisema wana uwezo wa kushinda. Lakini tunaamini hakuna anayeweza kuibuka mshindi, ndio maana tunachagiza kwa dhati suluhisho la kisiasa.”
Mkutano wa kwanza waGenevakuhusu amani nchiniSyriaulifanyika mwezi Juni mwaka jana.