UNAMA yalaani shambulizi lililolenga gavana wa kike nchini Afghanistan

9 Agosti 2013

Umoja wa Mataifa umelaani shambulizi la siku ya Jumatano nchini Afghanistan ambapo Seneta Rouh Gul Khairzad na watu kadha wa familia walijeruhiwa shambulizi ambalo pia lilisababisha kifo cha mwanae wa kike wa umri wa miaka minane na dereva wake.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA unasema kuwa Bi Khairzad na familia yake waliviziwa kwenye barabara kuu mkoani Ghazni alipokuwa ikielekea nyumbani kwenye mkoa wa Nimroz kusherehekea mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Naibu mwakilishi wa katibu mkuu nchini Afhanistan na UNAMA Nicholas Haysom anasema kuwa shambulizihiloni la kulaaniwa hasa wakati huu wa Idd ambao ni wakati wa amani. UNAMA imetuma rambi rambi zake na kumtakia nafuu ya haraka Bi Khairzad na wale wote walioponea shambulizihilo.