Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mswada wa msamaha Thailand waweza kuwaachilia wahalifu wakubwa:UM

Mswada wa msamaha Thailand waweza kuwaachilia wahalifu wakubwa:UM

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ina hofia kwamba mswada wa sheria ya msamaha ambao unajadiliwa bungeni wiki hii nchini Thailand.

Ofisi hiyo inasema endapo utapitishwa na kuwa sheria huenda ukawaachilia watu wenye makosa makubwa ya ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanyika wakati wa ghasia za kisiasa Aprili na Mai 2010.

Wakati wa machafuko hayo ofisi ya haki za binadamu inasema zaidi ya watu 90 walikufa na maelfu kujeruhiwa. Hapo Julai 6 mwaka 2010 serikali ya Thailand ilianzisha tume ya ukweli na maridhiano ambayo ilitoa ripoti iliyokusanya taarifa za makosa makubwa ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Ripoti hiyo ikapendekeza kuchukuliwe hatua za haraka ili kuhakikisha wale wote waliohusika na ukiukaji wa haki za binadamu wanachukuliwa hatua zinazostahili.