Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa dharura waombwa kwa tiba ya wapalestina watano

Msaada wa dharura waombwa kwa tiba ya wapalestina watano

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada kwa wakimbizi wa kipalestina, UNRWA limetoa ombi maalum wakati wa mfungo huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ya kusaidia kutoa fursa maalum ya maisha bora kwa wapalestina watano huko Lebanon ambao msaada wa dharura wa upasuaji kutokana na hali ya kiafya waliyonayo. George Njogopa na taarifa kamili. (TAARIFA YA GEORGE)

 Mpango huo wa usaidizi ulioanzishwa mnamo mwaka 2011, umefaulu kuleta tija baada ya wagonjwa 470 wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo saratani  kupata msaada wa kifedha.

Katika kipindi cha mwaka 2012, wakati kulipotolewa mwito wa msaada kwa ajili ya kugharimia matibabu kwa wagonjwa watatu kati ya wanne, UNRWA ilifanikisha matibabu hayo na sasa inaandaa mpango wa kuwagharimia wakimbizi wengine wanne wa Kipalestina waliokoLebanon.

Kila mwaka wastani wa Wakimbizi 4,000 wanakabiliwa na matatizo makubwa ya kiafya na hivyo kuhitaji kiasi kikubwa cha fedha  kwa ajili ya kugharimia matibabuyao.

Asilimia 95 ya wakimbizi wa Kipalestina walioko nchiniLebanonhawana bima za afya.Likishirikiana na mashirika mengine ya kihisani, UNRWA hugharimia matibabu ya msingi kwa wakimbizi hao.