Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchele uliongezewa nguvu waanza kusambazwa kwa wanavijiji Bangladesh

Mchele uliongezewa nguvu waanza kusambazwa kwa wanavijiji Bangladesh

Wanavijiji maskini nchini Bangladesh wameanza kupokea msaada wa mchele ulioongezewa nguvu za virutubisho ili kuwawezesha walaji kupata vitamin na madini.

Msaada huo unafuatia juhudi za pamoja za Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP, serikali ya Bangladesh na Serikali ya Uholanzi inayosaidiana na kampuni moja ya Sayansi ya DSM.

George Njogopa na taarifa kamili.

Viongozi wote wawili, Katibu Mkuu wa Wizara ya Wanawake na masuala ya watoto Tariq-ul Islam na mwakilishi wa shirika la chakula duniani WFP nchini Bangladesh Christa Rader leo walipata fursa ya kutembelea eneo la uzalishaji wa mchele na kituo kinachotumika kusambaza zao hilo kilichoko Kurigram .

Mchele huo ambao umeongezwa virutubisho ili kuongezwa nguvu unatajwa kuwa  ndiyo msingi mmojawapo wa vyakula vya wanga.

Kwa sasa husambazwa kwa kina mama wapatao 3,000 walioko kwenye mpango maalumu unaojulikana wanawake walioko kwenye makundi hatarishi.

Wanawake wengine 6,000 ambao tayari wameandikishwa na serikali wanatazamia kusambaziwa mchele huo katika kipindi cha wiki chache kuanzia sasa. Makundi mengine ya wanawake na wanaume watalazimika kwanza kupitia mpango wa hiari wa kukubali chakula hicho na ndipo wataanza kusambaziwa.

Kila mwaka Serikali ya Bangladesh husambaza msaada wa mchele kwa mamilioni ya watu ambao hali zao ni maskini  kupitia mpango maalumu ujulikanao huduma za ustawi wa kijamii kwa watu kipato cha chini.