IOM yaongoza usajili wa waliopoteza makazi kwa vita Sudani Kusini na DRC

30 Julai 2013

Kufuatia majadiliano ya kina ili kuruhusu kulifikia eneo lilioloathiriwa na vita jimboni Jonglei kusini kwa Sudan, mashirika ya misaada sasa yanaweza kufika eneo liitwalo Pibor ambapo mapigano kati ya jeshi la serikali na vikosi binafsi vyenye silaha, na mapigano ya kikabila yaliyozuka upya yameababisha wengi kukimbia miji na hivyo kusababisha maelfu ya kaya za wahamaji wanaotafuta hifadhi kusikojulikana au maeneo ambayo ni magumu kufikika kutokana na ukosefu wa usalama na mvua kubwa.

Shirika la uhamiaji duniania IOM kwa sasa linaongoza zoezi la usajili wa watu waliopoteza makazi kutokana na vita.

Katika mahojiano na Joseph Msami wa Radio ya Umoja wa Mataifa, msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe anaelezea pia kile shirika lake inakifanya katika kusadia zaidi ya kaya elfu mbili wanaotafuta makazi. Kwanza Bwana Jumbe anaanza kwa kueleza namna IOM inavyosajili raia wanaotafuta makaiz huko Sudani Kusini

(SAUTI JUMBE)