Colombia yatokomeza ugonjwa wa Usubi:WHO

30 Julai 2013

Shirika la afya duniani, WHO limethibitisha hatua ya Colombia kutokomeza ugonjwa wa macho aina ya Usubi unaosababishwa na minyoo, na hivyo kuwa nchi ya kwanza duniani kufikia hatua hiyo. Barua rasmi ya Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Margaret Chan, kwa serikali yaColombiaimetoa pongezi na kuitaka iendeleze ufuatiliaji thabiti ili kudhibiti mkurupuko wowote wa ugonjwa huo ambao bado unaendelea kutikisa mataifa mengine ya Amerika ya Kusini. Dkt. Carissa F. Etienne, Mkurugenzi wa chama cha afya kwa nchi za Amerika, PAHO amesemaColombiaimefanikiwa kutokomeza Usubi kutokana na jitihada shirikishi za miaka 16 zilizoongozwa na taasisi ya afya ya Taifa kwa usaidizi wa Wizara ya afya na zile za utafiti.

Harakati hizo zilihusika utoaji wa dawa za minyoo aina ya Ivermectin kwa wananchi mara mbili kwa mwaka kwa miaka 12 mfululizo bila kusahau elimu kwa umma na ushirikishaji wa wananchi kwenye kampeni hizo.

Usubi ni unashika nafasi ya pili kwa kusababisha upofu duniani na pia hufanya ngozi ya mgonjwa kuwa na vipele pamoja na malengelenge na huambukizwa na nzi aina ya Simulium anayepatikana maeneo ya mito.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter