Ban amezungumza na makamu wa Rais wa muda wa Misri:

29 Julai 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza kwa njia ya simu na makamu wa Rais wa mpito wa Misri Mohamed ElBaradei. Ban amemwelezea hofu yake kuhusu mwelekeo wa serikali ya mpito.

Amelaani vikali machafuko nchini humo ambayo yamepoteza maisha ya watu wengi. Ban ameitolewa wito serikali hiyo ya mpito kuchukua majukumu ya kuhakikisha maandamano yanafanyika kwa amani kwa WaMisri wote bila kujali itikadi zao za kisiasa na vyama wanavyoviunga mkono.

Katibu Mkuu amerejelea wito wake wa uongozi huo wa mpito kuanzisha mchakato wa amani wa kisiasa utakaojumuisha pande zote katika kusonga mbele nchini humo.Amesema kuwa kila vifo vinavyotokea vinazidisha ugumu wa maridhiano kwa taifa hilo.

Pia amerejea kutoa wito wa kuachiliwa kwa Mohammed Morsi na viongozi wengine wa Muslim Brotherhood au kesi zao kutathiminiwa ipasavyo.