Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wanne wafa maji Indonesia

Wahamiaji wanne wafa maji Indonesia

Wahamiaji wanne wamekufa maji katika kisiwa cha Java kilichoko Indonesia Mashariki wakati wakisafiri kwa njia ya boti kutoka nchini humo kuelekea Australia katika harakati za kutafuta hifadhi. Majeruhi wengine katika ajali hiyo wanatibiwa katika kambi ya wakimbizi nchini Indonesia na idadi ya vifo huenda ikaongezeka kufuatia hisia kwamba abiria katika boti hiyo walikuwa zaidi ya 157. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM:

(SAUTI YA JUMBE)