Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Swala la utekelezaji wa haki za watu wenye ulemavu laangaziwa

Swala la utekelezaji wa haki za watu wenye ulemavu laangaziwa

Mkutano unaongazia haki za watu wenye ulemavu ulioanza juzi unakamilika leo hapa Umoja wa Mataifa mjini New York. Mkutano huo ambao ni maandalizi ya mkutano mkuu wakati baraza  kuu la UM  litakapokutana mwezi september mwaka  huu pamoja na mambo mengine umegusia namna nchi wanachama wanavyotekeleza wajibu wao kuhusu haki ya kundi hilo.

Ungana na Joseph Msami katika makala hii itakayo kupa fursa ya kuelewa juhudi za UM katika kutekeleza makayaba juu ya haki za watu wenye ulemavu.