Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwajumuisha watu wenye ulemavu ni muhimu: wanaharakati

Kuwajumuisha watu wenye ulemavu ni muhimu: wanaharakati

Ikiwa dunia inataka kufanikiwa uwezo wake kamili , ni muhimu kuwajumuisha watu wote, wanaharakati wa haki za binadamu wamewaambiwa waandishi wa habari mjini New York jumatano.

Wanaharakati hao wameyasema hayo wakati wakiongea kuhusu mkutano wa siku mbili uanoangazia utekelezaji zaidi wa mkataba wa mwaka 2008, unaohusu haki za watu weneye ulemavu.

Balozi wa Kenya katika Umoja wa Mataifa  Macharia Kamau ni rais wa mkutano huo na amesema unakuja wakati huu ambapo dunia inajikita katika malengo ya maendeleo endelevu ambayo amesema yahusishe ujumuishwaji.