Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii nzima ya CAR imeathirika na mgogoro:Valarie Amos

Jamii nzima ya CAR imeathirika na mgogoro:Valarie Amos

Mratibu wa masuala ya kijamii na misaada ya dharura OCHA Bi Valarie Amos ambaye yuko ziarani Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) ameonya kwamba mgogoro wa kisiasa umeathiri taifa zima .

Bi Amos na mwenzie kutoka Jumuiya ya Muungano wa Ulaya wameitaka serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kurejesha mara moja utawala wa sheria ili msaada na fursa za kuwafikia waathiria zipatikane.

Bi Amos amesema watu wote wa taifa hilo milioni 4.6 wameathirika na machafuko wakiwemo watoto ambao ni nusu ya idadi hiyo., ameongeza kuwa mahitaji ya kibinadamu nchini humo ni makubwa na yanaongezeka ambapo watu milioni 1.6 wanahitaji msaada.

Akizungumza mjini Bangui, Bi Amos amesema usalama ni tatizo kubwa na Umoja wa Mataifa unajitahidi kurejesha uwepo wake na mipango yake katika maeneo malimbali ya nchi hiyo . Pia amesema hofu kubwa aliyonayo ni athari za machafuko hayo kwa wanawake na watoto.