Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

“Sober House” zaokoa vijana waliotumbukia kwenye madawa ya kulevya Zanzibar

“Sober House” zaokoa vijana waliotumbukia kwenye madawa ya kulevya Zanzibar

Ikiwa leo ni siku ya kupiga vita matumizi na usafirishaji wa madawa ya kulevya, huko Tanzania Zanzibar, yaelezwa kuwa vijana waliotumbukia katika matumizi ya madawa ya kulevya wanapatiwa misaada na makazi maalum ya kuwarekebisha tabia zao yajulikanayo kwa kiingerezakamaSober House.Mmoja wa wamiliki wa makazi hayo Bi. Fatma Musa Juma alizungumza na Stella Vuzo wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na kumueleza kile wanachofanya kusaidia vijana pamoja na changamoto. Kwanza aliuzwa je matumizi ya madawa hayo Zanzibar ni sugu?