Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya inasema itahakikisha malengo ya mileniwa yanafikiwa kama sio asilimia 100 basi hata 50

Kenya inasema itahakikisha malengo ya mileniwa yanafikiwa kama sio asilimia 100 basi hata 50

Serikali ya Kenya imesema itajitahidi kwa kila hali kutimiza malengo ya milenia ifikapo 2015.

Waziri wa Afya wa Kenya Beth Mugo akizungumza na Flora Nducha amesema hata kama hawatofikia asilimia 100 lakini watahakikisha wanafikia hata nusu. Beth Mugo ambaye amekuwa New York kwa ajili ya mkutano wa tathimini ya hatua zilizopigwa kufikia malengo ya maendeleo ya milenia na pia mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa amesema nchi yake imepiga hatua kubwa.

Amesema hasa katika lengo namba nne kupunguza vifo vya watoto, namba tano kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na wakati wa kujifungua na namba sita kupambana na ukimwi, malaria na maradhi mengine wamepiga hatua na wana imani kubwa watazidi asilimia 50, Wasikilize.