Nusu ya kambi za wakimbizi wa Kipalestina nchini Syria zimegeuka kuwa “ Tamthilia ya vita”

17 Juni 2013

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi wa Palestina UNRWA ameuambia mkutano wa wadau kuwa, wakimbizi saba wa Kipalestina kati ya 12 wamegeuka kuwa “ Tamthilia ya vita”

Filippo Grandi amesema kuwa vitendo kama kubakwa, kunyanyaswa, kutekwa, hofu ya maisha ikiwa sehemu ya maisha yao ya kila siku.

Akizungumza Mjini Amman katika mkutano wa pili wa kila mwaka wa shirika hilo, Grandi amesema kuwa zaidi ya wakimbizi 530,000 wa Kipalestina ambao walioandikishwa nchini Syria wanaaminika kuingia mtawanyikoni na kiasi cha asilimia 15 cha wakimbizi wote wamekwenda katika mataifa mengine.

Kulingana na Grandi,raia wa Misri nao wameanza kuwahifadhi wakimbizi wa Kipalestina wanaotoka Syria na baadhi yao wameingia Gaza.