Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wapalestina elfu Tano wanaoshikiliwa Israel wanaishi maisha dhalili

Wapalestina elfu Tano wanaoshikiliwa Israel wanaishi maisha dhalili

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa ametaka kuundwa kwa tume ya kuchunguza hali ya takribani wapalestina Elfu Tano wanaoshikiliwa au kufungwa nchini Israel kwa madai kuwa maisha yao ni dhalili na ya taabu. Taarifa ya George Njogopa inafafanua zaidi.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Richard Falk ambaye ni mtaalamu huru wa masuala ya haki za binadamu kwa Mamlaka ya Palestina amesema kuwa raia wengi wa taifahilowalioko kwenye magereza yaIsraelwanaandamwa na vitendo vya uovu ikiwemo kuteswa, kunyimwa haki kupata msaada wa kisheria na wakati mwingine familia zao zinapigw amarafuku kuwatembelea.  Katika ripoti yake aliyoiwasilisha mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa Bwana Mr Falk amesema kuwa vitendo viovu vinavyowakumba watoto wa Kipalestina walioko kwenye magareza ya kijeshi yaIsraelsasa vinavuka mipaka na hufanywa kwa mtindo wa kupangiliwa.

 

(SAUTI YA RICHARD)