Vyombo vya habari matatani Burundi

8 Juni 2013

Nchini Burundi, serikali imepitisha sheria mpya ya vyombo vya habari. Mengi yameibuka baada ya Rais Pierre Nkurunzinza kutia saini sheria hiyo kutokana na kile kinachoelezwa kuwa kinabana vyombo vya habari na kuweka vikwazo kwa uhuru wa kujieleza na kupata habari ambavyo ni moja ya haki za msingi za binadamu.

Tayari Umoja wa mataifa kupitia katibu Mkuu Ban Ki-Moon umetaka Burundi kuangalia upya hatua hiyo kwani ni ya kusikitisha. Mathalani  yaelezwa waandishi wa habari kwa mujibu wa sheria mpya wanapaswa kufichua vyanzo vyao vya habari na kubwa zaidi faini kwa makosa ya uandishi wa habari imeongezwa kwa asilimia Mia Mbili.

Je kulikoni? Basi ungana na mwandishi wetu wa maziwa makuu kutoka mjini Bujumbura, Ramadhani Kibuga.

(MAKALA NA RAMADHAN KIBUGA)