Vikwazo vya Israel ni kizingiti cha uchumi wa Palestina ILO

6 Juni 2013

Uchumi kwenye utawala wa Palestina hautaboreka hadi pale Israeli itakapoondoa vikwazo ilivyoweka kwa mujibu wa Shirika la kazi duniani ILO.Alice Kariuki anaeleza.(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)Kupitia kwa ripoti yake ya kila mwaka kuhusu hali ya wafanyikazi kwenye maeneo ya kiarabu yaliyokaliwa ILO inasema kuwa uchumi wa Palestina unajikikota kukua huku kukiwa na ukosefu mkubwa wa ajira, umaskini na uhaba wa chakula.

Ripoti hiyo inasema kuwa ujenzi wa makao zaidi unazuia uchumi wa palestina hasa kwenye sekta ya binafsi. Kari Tapiola ni mshauri kwa mkurugenzi mkuu wa ILO.

“Israel haihitaji tu kutupilia mbali vikwazo kwa watu na biashara lakini inastahili kutupilia mbali kila kitu ili uchumi wa Palestina  uweze kukua na kuleta ajira za  kisasa. Kuendelea kutwaliwa kwa ardhi kunazuia sekta za kibinafsi kupiga hatua . Na ikiwa hali ya kukaliwa kwa ardhi itaendelea kuwa kizuizi kwenye jitihada za ukuaji kwa uchumi wa Palestina suala la kuwepo mataifa mawili litasamabaratika.”