Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ampongeza Rice, aelezea uthabiti wake

Ban ampongeza Rice, aelezea uthabiti wake

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amempongeza Bi Susan Rice kufuatia kuteuliwa kwake kuwa mshauri wa usalama wa taifa wa serikali ya Marekani .

Bwana Ban amempongeza Rice kwa utendaji wake mzuri wakati akitumika katika nafasi ya mwakilishi wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2009 akimtaja kama sauti kuu katika baraza la usalama la umoja huo na ushauri madhubuti juu ya maswala mbalimabli yakiwemo amani na usalama, haki za binadamu na maendeleo.

Katibu Mkuu amesema katika taarifa yake kuwa amenufaika pakubwa kutokana na msaada wake na ushauri pamoja na kumuelezea namna alivyounga mkono maswala ya Afrika hususani uwezeshwaji wa wanawake na kwamba Umoja wa Mataufa kwa ujumla umenufaika.