Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yawasaidia wahamiaji wa Ethiopia kuondoka Somalia

IOM yawasaidia wahamiaji wa Ethiopia kuondoka Somalia

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, limesaidia kurejesha nyumbani watu arobaini na wawili, raia wa Ethiopia waliokuwa wamekwama Hargeisa, kwenye jimbo la Somaliland nchini Somalia.

Wengi wa watu hao waliokwenda kutafuta makao kwenye kituo cha IOM cha kuwasaidia wahamiaji, ama walikuwa wagonjwa au wamedhulumiwa na walanguzi na wasafirishaji haramu. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)