Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chanjo zatolewa CAR, fedha zaidi zahitajika: OCHA

Chanjo zatolewa CAR, fedha zaidi zahitajika: OCHA

Licha ya Wabia wa afya kufanikiwa kutoa chanjo kwa takribani watoto laki moja na elfu 23 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, bado uhaba wa fedha ni changamoto kubwa wakati ambapo misaada ya kibinadamu inahitajika.Joseph Msami na taarifa kamili(RIPOTI YA JOSEPH MSAMI)

Kiasi cha dola millioni 139 zinahitajika ili kutoa misaada ya binadamu, wakati ambapo bado ukosefu wa fedha ni asilimia 31.Mfuko Mkuu wa mahitaji ya dharura CERF, umetenga dola milioni 7 ikiwa ni dharura ya kuokoa maisha ya watu milioni 1.1 kutoka Umoja wa Mataifa na wabia wengine.

Mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Kaarina Immonen,amesema fedha hizo zitatumiwa kutoa misaada ya chakula na madawa,maji ya bomba, usafi wa mazingira,msaada wa kisaikolojia kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia , usimamizi wa taka na huduma za afya ya uzazi.

Yens Laerke ni msemaji wa OCHA

(SAUTI YA YENS)