Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ngumu na kukosekana kwa usalama kunafanya wakimbizi wengi kushindwa kwenda Lebanon-UNHCR

Hali ngumu na kukosekana kwa usalama kunafanya wakimbizi wengi kushindwa kwenda Lebanon-UNHCR

Huku mapigamo yakizidi kuchacha katika eneo la Al Qusayr nchini Syria, Dhirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuwa limeshuhudia wakimbizi wachache wakivuka mpaka na kuwasili Mashariki mwa Lebanon.

 Maafisa wa shirika hilo wamesema kuwa kuna uwezekano wa kufunguliwa njia mpya inayotumiwa na wakimbizi hao kuelekea eneo la Arsal nchini Lebanon wakitokea Qusayr.

 Hata hivyo kutokana na mapigano makali yanayoendelea kuna uwezekano pia raia wengine wamekwama katika miji ya mbalimbali ikiwemo miji ya Qara, Nabek, na Hasyah.

Wakimbizi hao walioko Lebanon wameelezea hali ngumu wanazokumbana nazo ikiwemo shida wanazozipata wakati wakiwa safarini.