Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yemen yaendelea kukabiliwa na hali ngumu ya kibinadamu

Yemen yaendelea kukabiliwa na hali ngumu ya kibinadamu

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa taifa la Yemen linaendelea kukabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu. Ukosefu wa mahitaji kama chakula, mafuta na hali ngumu ya kiuchumi vimeongeza umaskini zaidi nchini Yemen na kwa watu ambao tayari wanakabiliana na njaa na utapiamlo.

Kwa sasa WFP inafanya mikakati ya kulisha watu milioni 3.5 ambao wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula nchini Yemen kutokana na kuongezeka kwa bei ya vyakula na ambao wamehama makwao kaskazini na kusini mwa nchi. Inaripotiwa kuwa hata baada ya kutokea hali hiyo tayari zaidi ya asilimia 50 ya watoto nchini Yemen wanasumbuliwa na utapiamlo kama anavyofafanua msemaji wa WFP Gaelle Sevenier

(SAUTI YA GAELLE SEVENIER)