Uhuru wa kujieleza ni haki ya kila mtu:UM
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika kuchagiza na kulinda haki ya uhuru wa maoni na kujieleza Frank La Rue amesema serikali lazima zichangie na kuleta mabadiliko badala ya kukandamiza watu.
Akitoa ujumbe maalumu wa kuadhimisha siku ya uhuru wa vyomvo vya habari itakayoadhimishwa Mai 3, kwamba hivi sasa matukio mengi yanajiri Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini ambapo watu hususani vijana kwa pamoja wamesimama kidete ili kupinga miongo ya ukandamizaji na kunyimwa haki za msingi za binadamu.
La Rue amesema anawapongeza watu hao wakiwemo waandishi wa habari, wanaharakati, kwa ujasiri wao wa kudai mabadiliko, demokrasia, uwazi na haki. George Njogopa anaripoti.
(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)