Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaonya kuhusu kuwepo mikurupuko ya magonjwa nchini Syria na mataifa jirani.

WHO yaonya kuhusu kuwepo mikurupuko ya magonjwa nchini Syria na mataifa jirani.

Shirika la afya duniani limeelezea hisia zake kutokana na kuendelea kuongezeka kwa visa vya magonjwa ya kuambukiza nchiniSyriana pia mionghoni mwa wale waliolazimika kuhama makwao walio kwenye mataifa jirani likionya kuwa bila ya hatua za kuzuia magonjwa hayo huenda kukazuka  madhara makubwa.

Kwa muda wa miaka miwili mifumo ya afya nchiniSyriaimesambaratika ambapo karibu asilimia 35 ya hospitali za umma zikiwa hazitoi huduma kabisa huku asilimia 70 ya watoa huduma za afya kwenye sehemu zingine wakiwa tayari wamekimbia hali ambayo imesababisha kuwa na upungufu mkubwa wa watoa huduma za afya.