Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya UM yaelezea wasiwasi wake kutokana na matumizi ya nguvu nchini Uturuki

Ofisi ya UM yaelezea wasiwasi wake kutokana na matumizi ya nguvu nchini Uturuki

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea wasi wasi wake kufuatia kuwepo kwa matumizi ya nguvu kutoka kwa maafisa wa usalama dhidi ya waandamanaji nchini Uturuki.Ofisi ya haki za binadamu inakaribisha dhibitisho kutoka kwa serikali kuwa huenda nguvu zimetumika lakini pia imetoa wito wa kutaka kufanyika kwa uchunguzi kuhusu sualahilona kuwachukulia hatua wahusika. Cecille Poullie ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa

(SAUTI YA CECILLE POULLIE)