Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ethiopia yachukua hatua kudhibiti homa ha manjano

Ethiopia yachukua hatua kudhibiti homa ha manjano

Nchini Ethiopia, wizara ya afya wiki ijayo inaanza kampeni ya dharura ya utoaji chanjo dhidi ya homa ya manjano baada ya kuthibitishwa kuwepo kwa wagonjwa Sita tarehe Saba mwezi wa Mei.

Kampeni hiyo inalenga kufikia zaidi ya watu Laki Tano maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.

Kundi la kimataifa la kuratibu utoaji chanjo dhidi ya homa ya manjano litatoa dozi zaidi ya Laki Tano na Elfu Themanini kwa kampeni hiyo inayoungwa mkono na serikali ya Ethiopia na ubia wa chanjo duniani GAVI.

Kwa upande wake shirika la afya duniani, WHO linasaidia kwa karibu uchunguzi, na kuwajengea uwezo watumishi wa afya nchini humo pamoja na kufuatilia harakati za kinga na utabibu kwenye maeneo yenye ugonjwa huo.