Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iran na taasisi ya Cameroon wapata tuzo ya UM

Iran na taasisi ya Cameroon wapata tuzo ya UM

Mtaalamu mmoja wa takwimu za jamii raia wa Iran anayeshughulikia masuala ya maendeleo na afya ya uzazi pamoja na taasi inayotoa mafunzo juu ya masula ya afya ya uzazi wameshinda tuzo la idadi ya watu la Umoja wa Mataiafa.

Tuzo hilo lilibuniwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1981 na hutolewa kila mwaka kwa watu na taasisi kwa kuchangia katika masuala ya idadi ya watu na suluhu zinazohitajika. Tuzo la mwaka huu lilimwendea Mohammad Jalal Abbasi-Shavazi mwenyekiti wa idara ya kuchunguza idadi ya watu kwenye chuo kikuu cha Tehran pamoja na taasisi moja nchini Cameroon ya (IFORD).

Bwana Abbasi-Shavazi ana ujuzi wa miaka mingi kama mwalimu , katika masuala ya idadi ya watu , afya ya uzazi , uhamiaji na kuhusu wakimbizi. Nayo taasisi ya IFORD iliyobuniwa mwaka 1972 imekuwa ikiongoza kwa kutoa mafunzo kuhusu masuala ya idadi ya watu ikihudumia nchi 26 barani Afrika.