Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chanjo dhidi ya polio yaanza nchini Somalia

Chanjo dhidi ya polio yaanza nchini Somalia

Maafisa wa afya nchini Somalia wameanzisha kampeni ya siku tatu inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ya kuwachanja zaidi ya watoto milioni 1.8 dhidi ya ugonjwa wa Polio miaka minne baada ya taifa hilo kutangazwa kutokuwa na ugonjwa huo.

Kampeni hiyo unayoendeshwa na wafanyikazi wa afya nchini Somalia kwa ushirikiano na shirika la afya duniani WHO na lile la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataiafa UNICEF pamoja na mashirika mengine ina lengo la kumfikia kila mtoto nchini humo.

Mwakilishi wa WHO nchini Somalia Marthe Everard anasema kuwa kisa cha mwisho cha Ugonjwa wa Polio kiliripotiwa mwezi machi mwaka 2007 baada ya juhudi za kimataifa za kumaliza ugonjwa huo nchini humo.

Awamu mbili za kutoa chanjo hiyo zinatarajiwa kuendeshwa nchini Somalia mwaka huu zinazolenga kuwafikia watoto 800,000 ambao hawakupata chanjo hiyo mwaka uliopita.