Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Magonjwa ya mifugo ni changamoto kubwa kwa wafugaji

Magonjwa ya mifugo ni changamoto kubwa kwa wafugaji

Ni mpakani mwa Uganda na Kenya, eneo lililo ndani zaidi ambapo jamii ya hapa inategemea zaidi mifugo kwa maisha yao. Katika kusaka malisho na maji ya mifugo, mara kwa mara wachungaji wanavusha mpaka mifugo hiyo ambayo ni mbuzi na ng’ombe.Miongoni mwa wafugaji wa eneo hili ni Cholima Logid, baba wa watoto Tisa ambaye amekuwa akivusha mifugo yake lakini alikabiliwa na changamoto.

(SAUTI YA Cholima Logid)

Magonjwa huvuka mpaka kirahisi. Wafugaji wanaweza kutegemea tu huduma za mifugo zinazotolewa kule wanakofikia iwe ni Uganda au Kenya. Kama kama Moroto, Uganda ambako mashirika ya hapa yanaendelea na ukaguzi wa mara kwa mara wa mifugo.

SAUTI Kennedy Ojuang, C&D lab assistant:

Lakini kuna tofauti za ubora na bei ya huduma za tiba kwa mifugo zinazotolewa katika pande mbili hizo za mpaka. Na ukosefu wa uratibu wa huduma hizo unakwamisha harakati za kudhibiti milipuko ya magonjwa ya mifugo.

(SAUTI Emmanuel Isingoma)

Lakini msaada wa Umoja wa Ulaya na shirika moja la ECHO, umechochea mamlaka ya pamoja ya maendeleo ya nchi za pembe ya Afrika IGADA na FAO na mashirika mengine kuanzisha programu ya kuboresha afya ya mifugo pande mbili za mpaka. Makubaliano yalitiwa saini kati ya serikali ya Uganda na Kenya mwezi Aprili mwaka huu. Katibu mtendaji wa IGAD Balozi Mahboub Maalim anasema mpango huo utakuwa ni mfano.

(SAUTI Ambasador Mahboub Maalim)

Na kwa wananchi ni furaha….

(Ngoma wananchi)

(MAKALA SAUTI YA JOSEPH MSAMI)