Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO yachochea usawa maofisini kwa waliobadili jinsi na wapenzi wa jinsia moja

ILO yachochea usawa maofisini kwa waliobadili jinsi na wapenzi wa jinsia moja

Shirika la kazi duniani, ILO limesema linaongeza kasi ya kutokomeza vitendo vya watu kubaguliwa kazini kwa misingi ya mwelekeo wao wa jinsia au mapenzi.Mkurugezi Mkuu wa ILO Guy Rider amesema hatua za kuhakikisha usawa kwa wanawake na walemavu sehemu za kazi zimeonyesha matumaini na maendeleo yaliyopatikana kuhakikisha mashoga na waliobadili jinsia wanapata haki sawa kwenye kazi hayana mjadala.

Hata hivyo amesema bado kuna changamoto na ametaka nchi wanachama kutumia vigezo vya kimataifa ya ajira kutokomeza ubaguzi huo sehemu ya kazi.