Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yajiandaa kuwapelekea misaada wakimbizi nchini Chad

UNHCR yajiandaa kuwapelekea misaada wakimbizi nchini Chad

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linandaa misaada kwa maelfu ya wakimbizi kutoka jimbo la Darfur walioingia mashariki mwa Chad wakati hofu ikitanda kuwa mvua zinazonyesha huenda zikazuia kufikiwa kwa eneo hilo. Hivi majuzi karibu watu 30,000 walikimbia ghasia za kikabila kaskazini na magharibi mwa Darfur nchini Sudan. Taarifa ya Alice Kariuki inaarifu zaidi

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Wengi wa wakimbizi hao ni wanawake na watoto na kwa sasa wanahitaji kwa dharura makao, chakula maji safi na huduma za matibabu. Wanasema kuwa walikimbia makwao kwa sababu watu walikuwa wakiuawa wakati wa ghasia hizo huku nyumba nyingi zikiteketezwa moto na watu waliokuwa wamejihami. Kundi la kwanza la wakimbizi kutoka Sudan walioanza kuwasili eneo la Tissi mashariki mwa Chad kati ya mwezi Januari na machi wakati mizozo kuhusu migodi ya dhahabu eneo la Jabel Amer kaskazini mwa Darfu iligeuka na kuwa ghasia za kikabila kati ya kabila la Ban Hissein na Rizeigat. Ghasia hizo pia ziliwalazimu karibu raia 20,000 wa Chad kukimbia na kuingia eneo la Tissi wakiwemo wakimbizi 458 kutoka Jamhuri ya Afrika ya kati ambao wamekuwa wakiishi kwenye jimbo la Darfur kwa miaka mingi.