Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ateua wawakilishi wake maalum huko Mali na Cote D’Ivoire

Ban ateua wawakilishi wake maalum huko Mali na Cote D’Ivoire

Ujumbe wa umoja wa mataifa wa kuweka utulivu huko Mali, MINUSMA ulioanzishwa mwaka huu umepata kiongozi ambaye pia atakuwa mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon, naye si mwingine bali ni Bert Koenders kutoka Uholanzi. Bwana Koenders anaenda kushika wadhifa huo akitokea hukoCote D’Ivoirealikokuwa akimwakilisha katibu Mkuu kwenye ofisi ya Umoja huo, UNOCI tangu Oktoba mwaka 2011.  Mkuu huyo wa ujumbe huo mpya wa MINUSMA ana uzoefu wa miaka 25 ya siasa za kitaifa, masuala ya kimataifa na maendeleo na amewahi kushika nyadhifa mbali mbali ikiwemo Waziri wa ushirikiano wa maendeleo wa Uholanzi. Wakati huo huo, Katibu Mkuu Ban Ki-Moon amemteua Bi. Aichatou Mindaoudou kutokaNigerkuwa mwakilishi wake maalum hukoCote D’Ivoireakiongoza ofisi ya umoja huo UNOCI, iliyoachwa wazi na Koenders.  Bi. Mindaoudou ameshika nyadhifa kadhaa ndani ya serikali yaNigerna ndani ya Umoja wa Mataifa ikiwemo Kaimu mkuu wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika hukoDarfur, UNAMID tangu Agosti 2012 hadi Machi mwaka huu.