Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaongeza msaada wa chakula kaskazini mwa mali

WFP yaongeza msaada wa chakula kaskazini mwa mali

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linaongeza operesheni zake za msaada wa dharura Kaskazini mwa Mali na hususani maeneo ya Timbuktu, Gao na Kidal.Katika maeneo hayo moja kati ya kila familia tano inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

WFP inasema kufikisha misaada ya kibinadamu katika maeneo hayo bado ni changamoto na inatathiminiwa kila siku na Umoja wa Mataifa na washirika wake. Mwezi Machi mwaka huu WFP imetoa msaada wa dharura wa chakula kwa watu zaidi ya 278,000 Mali.