Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ITU yachukua hatua kulinda watoto dhidi ya matumizi mabaya ya intaneti

ITU yachukua hatua kulinda watoto dhidi ya matumizi mabaya ya intaneti

Washiriki wa mkutano wa shirika la kimataifa la mawasiliano, ITU wamechukua hatua kulinda watoto dhidi ya intaneti ikiwa ni sehemu ya mwelekeo wa kuhakikisha dunia inanufaika na jamii habari ifikapo mwaka 2015. Assumpta Massoi ana maelezo zaidi.

 (TAARIFA ASSUMPTA)

Katika kutekeleza hatua hiyo, mkutano huo umemteua Dame Jonathan ambaye ni mke rais wa Nigeria kuwa balozi mwema wa mpango wa kuwalinda watoto dhidi ya athari hizo ujulikanao kama Child on  line.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum na kituo hiki kutokaGeneva, mwakilishi wa Tanzania katika mkutano huo Koni Shirima amesema kupitia mpango huo watoto wanaelimishwa namna ya kufaidika na mitandao hususani kuwasaidia katika kujenga utamaduni hasa kwa kuzingatia ugumu wa kuepukana na teknolojia ambayo imekuwa kwa kasi.

Halikadhalika wawakilishi wa makampuni yanayoandaa programu za komputa wanajadili nan kupata maelekezo  juu ya namna ya kuwalinda watoto ambao wanatajwa kama waathirika wakuu wa Teknohama.

 (SAUTI KONI SHIRIMA)