Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Brigedi ya kuingilia kati yaanza kuwasili mashariki mwa DRC: MONUSCO

Brigedi ya kuingilia kati yaanza kuwasili mashariki mwa DRC: MONUSCO

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, MONUSCO, umesema kuwa kikosi cha awali cha watu 45 kutoka kwa Brigedi yake ya kuingilia kati kimewasili mjini Goma hii leo.

Brigedi hiyo iliundwa kufuatia azimio la Baraza la Usalama la Machi 28 mwaka huu wa 2013.

Brigedi hiyo itatekeleza majukumu yake ya kuvunja na kupokonya silaha makundi yalojihami huko mashariki ya DRC, chini ya kamanda wa kikosi cha MONUSCO.

Vikosi vilosalia vya Brigedi hiyo vinatarajiwa kupelekwa mashariki mwa DRC katika siku na wiki chache zijazo