Kazi niliyotumwa Somalia nimeimaliza kwa wakati na kwa amani-Balozi Mahiga
Baada ya miaka mitatu ya kuhudumu kama Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Balozi Augustine Mahiga amesema jukumu hilo lilikuwa ni kubwa na changamoto nyingi. Lakini alisonga mbele hadi kuwezesha kuundwa kwa serikali, bunge na katiba nchini humo. Balozi Mahiga ambaye anahitimisha jukumuhilomwezi ujao wa Juni, alisema hayo katika mahojiano maalum na Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa ambapo katika sehemu hii ya kwanza anaanza kwa kuzungumzia alivyopokea jukumu hiloJuni 2010.