Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na Somalia wasaini makubaliano ya kuzuia ukatili wa kingono

UM na Somalia wasaini makubaliano ya kuzuia ukatili wa kingono

Katika kuongeza jitihada za kuzuia vitendo vya ukatili wa kingono nchiniSomalia, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson na Rais Hassan Sheik Mohamoud wametiliana saini makubaliano ya pamoja hukoLondondhidi ya vitendo hivyo. Makubaliano hayo pamoja na mambo mengine yanataka kuwachunguza watu wote wanaojumuishwa katika vikosi vya usalama vya Taifa ili kuhakikisha kwa dhati wanatetea haki za binadamu na kwamba hawajawahi kukiuka haki za binadamu. Halikadhalika kuhakikisha ulinzi wa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kingono na pia mashuhuda wanaotoa ripoti na hata waandishi wa habari wa matukio hayo. Bwana Eliasson amesema amesema kivitendo ina maana hatua hiyo ni kuwafikisha watekelezaji wa vitendo hivyo mbele ya sheria, kutoa msaada kwa wahanga na kuhakikisha mfumo wa haki una uwezo wa kushughulikia vitendo hivyo.  Mjumbe maalum wa Katibu mkuu dhidi ya ukatili wa kingono Hawa Zainab Bangura ameunga mkono hatua hiyo na kusema ofisi yake itaendelea kushirikiana na serikali yaSomaliakuzuia ukatili wa kingono.